Quran ni hazina ya hekima na inatoa suluhisho la vitendo kwa matatizo ya wanadamu. Ni mwongozo kwa wale walio na imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu na yale aliyoyafunua kwa Mtume Muhammad (amani iwe juu yake). Mwenyezi Mungu (SWT) anaielezea mwanzoni mwa Surah Al-Baqara kama "... mwongozo kwa wale walio Al-Muttaqun [waumini wacha Mungu wa Tawhidi ya Kiislamu…..".
Sehemu hii inajumuisha aya zilizochaguliwa kutoka kwa Quran ambazo unaweza kuzitafakari na kunufaika nazo kwa kuzitumia katika nyanja mbalimbali za maisha. Tafakari hiyo inalenga kuangazia jinsi Allah (SWT) anavyotutarajia sisi kurejea Kwake, kujikurubisha Kwake, na kuyatengeneza maisha yetu kulingana na mafundisho ya Mtume Muhammad (saw). Dakika chache za kutafakari zinaweza kusaidia katika kuimarisha ufahamu wako wa hekima ya Kimungu.